Hadithi Yako ya Kweli (Your True Story, Swahili Translation)

Mwongozo Muhimu wa Siku 50 Kwa Ajili ya Maisha Yako Mapya Pamoja na Yesu

Susan Freese

EPUB
9,49
Amazon iTunes Thalia.de Weltbild.de Hugendubel Bücher.de ebook.de kobo Osiander Google Books Barnes&Noble bol.com Legimi yourbook.shop Kulturkaufhaus ebooks-center.de
* Affiliatelinks/Werbelinks
Hinweis: Affiliatelinks/Werbelinks
Links auf reinlesen.de sind sogenannte Affiliate-Links. Wenn du auf so einen Affiliate-Link klickst und über diesen Link einkaufst, bekommt reinlesen.de von dem betreffenden Online-Shop oder Anbieter eine Provision. Für dich verändert sich der Preis nicht.

All In Ministries Books img Link Publisher

Geisteswissenschaften, Kunst, Musik / Religion/Theologie

Beschreibung

JINUNULIE KIMOJA. MNUNULIE MTU KIMOJA KAMA ZAWADI.* Maisha yako yanaweza kubadilika ndani ya Siku 50. Zana hii KAMILI ya Kujifunza Biblia ina mambo muhimu juu ya uanafunzi kwa ajili ya Wakristo wapya ulimwenguni kote (hakuna mifano ya kimagharibi). Ni vigumu kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu na kutimiza kusudi lako bila ufahamu mzuri wa hadithi Yake na sehemu yako katika hadithi hiyo.
Masomo haya 50 ya kila siku yanafunua MAMBO MUHIMU YA IMANI ili kufanya urafiki wako na Yesu uwe wa kina na kukupa UJUZI WA KIUTENDAJI ili iwe mfuasi Wake.
Jifunze kile ambacho waumini wakomavu wamejua kwa miaka mingi ndani ya Siku 50 kupitia safari hii rahisi lakini inayobadilisha maisha.
Wiki ya 1:    Hadithi ya Mungu—Kugundua hadithi kuu ya Biblia
Wiki ya 2:    Hadithi Yako—Kukumbatia utambulisho wako mpya katika Kristo
Wiki ya 3:    Kusudi Lako—Kutimiza kusudi la maisha yako
Wiki ya 4:    Kukaa Ndani—Kubaki Ukiwa Umeunganishwa  na Mungu
Wiki ya 5:    Neno la Mungu—Kumsikiliza Mwanzilishi wa Uzima
Wiki ya 6:    Neno la Mungu—Kunena na Mwanzilishi wa Uzima
Wiki ya 7:    Roho Mtakatifu—Kutimiza Hadithi Yako Kwa Nguvu Za Mungu
Kila wiki utajifunza zaidi juu ya simulizi ya Biblia.
Utagundua siri za maisha ya Kikristo, kama vile jinsi ya kukaa ndani ya Kristo, kushughulikia shaka, kupinga majaribu, na kumwabudu Mungu katika misimu ya mateso.
Pia utajifunza njia za kiutendaji za kujifunza Biblia yako, kushiriki imani yako, kufanya wanafunzi, na kuomba. Ikiwa hujaanzisha uhusiano na Yesu, utapata fursa ya kuchukua hatua hiyo.
Kila siku inatamatishwa kwa mbinu ya Amri Kuu ya kutumia Maandiko, maswali, maombi, na mahali pa kuchukua hatua zako zinazofuata.
KITABU HIKI NI KWA AJILI YAKO IKIWA:
- Wewe ni muumini mpya katika Yesu unayetafuta hatua zinazofuata za kukuza imani yako,
- Wewe ni Mkristo anayetafuta kufundishwa kuwa mwanafunzi au kuwafundisha wengine kuwa wanafunzi,
- Unachunguza Ukristo na unataka kujua jinsi ya kuwa mfuasi wa Yesu.
KILE AMBACHO WASOMAJI WANASEMA:
“Ni safari INAYOBADILISHA MAISHA.” Scott Ray, IMB
“Mojawapo ya ZANA BORA ZAIDI za UANAFUNZI ambazo nimewahi kusoma.” Chris Price, Mchungaji wa Chets Nocatee
“Najua KITAKUTIA MOYO.” Dkt. Richard Blackaby, mwandishi mwenza wa Experiencing God
“Kitabu ambacho ni LAZIMA KISOMWE na Wakristo wapya, huku kikitoa CHANGAMOTO kwa Wakristo wakomavu zaidi.” Mac Heavener, Trinity Baptist College
“Zana ya uanafunzi iliyo kamili, RAHISI KUELEWEKA na sahihi kitheolojia.” Kelley Hastings, Mchungaji wa Wanawake
“Inaunganisha pamoja injili ya uanafunzi na MWONGOZO WA NYANJANI WA KUFANYA WANAFUNZI unaoweza kutumiwa na watu wote katika maeneo mbalimbali.” Bob Bumgarner, mwanamkakati mkuu wa kimisionari
“Ni MAFUNDISHO YA KINA ambayo yatajibu maswali yako mengi kuhusu safari yako ya kiroho.” Betzaida Vargas, mwanzilishi wa Samaritana del Pozo
MAISHA YAKO YANA HADITHI MPYA YA KUSIMULIA:
Shuhudia imani ya kweli na furaha unapotumia kweli takatifu kubadilisha maisha yako. Kukutana na Yesu ni mwanzo tu. Kumfuata--hivyo ndivyo hadithi yako ya kweli inavyojitokeza.
--Maneno muhimu, maswali ya kutafakari ya kibinafsi ya kila siku na ya majadiliano ya kikundi ya kila wiki yamejumuishwa.
-- Kimeandikwa kwa ajili ya wasomaji kutoka kote duniani bila mifano ya kimagharibi.
--Zaidi ya saa 10,000 za utafiti, hakiki 3 za kitheolojia, marejeo zaidi ya 1,400 ya kibiblia, wasomaji zaidi ya 50 wa kutoa maoni ya awali = Safari 1 Inayobadilisha Maisha.
Taarifa zaidi zinapatikana kwenye yourtruestorybook.com
* JINUNULIE KIMOJA. MNUNULIE MTU KIMOJA KAMA ZAWADI. Mapato kutoka kwa kila kitabu kinachouzwa yatatoa nakala iliyotafsiriwa kwa muumini ambaye hana nyenzo za kutosha katika nchi inayoendelea.

Weitere Titel in dieser Kategorie
Cover Kupaa Kama Tai
Thomas Gregory Stewart
Cover Vitengo vya Ujenzi
Teresa and Gordon Skinner
Cover Uanzishaji Wa Imani
Teresa and Gordon Skinner

Kundenbewertungen